Sunday 10 May 2015

Eeeeehh eti Di Maria kufungasha virago vyake OT..............

  

Manchester United imemsajili winga wa PSV Memphis Depay kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu na huenda ikamtema mchezaji waoAngel Di Maria.
Lakini klabu ya Paris Saint-Germain ‘PSV’ ya Ufaransa imesema ipo tayari kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo kama ataruhusiwa na uongozi wa timu yake ili kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.
Mchezaji huyo alisajili kwa pauni milioni 60 akitokea Real Madrid lakini hakuonyesha kiwango kizuri msimu huu na kuwa hatarini kutemwa.
Man United awali ilitaka kumuuza mchezaji huyo lakini baadaye meneja wa timu hiyo Luis Van Gaal alibadili mawazo na kudai ataendelea kubaki kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mwingine.

Kwahabari motomoto za kimichezo toka nje na ndani ya nchi, usikose kututembelea ALIWANTZ wakali wa burudani Tanzania

No comments:

Post a Comment